Romans 7:7-12

7 aTuseme nini basi? Kwamba sheria ni dhambi? La, hasha! Lakini, isingekuwa kwa sababu ya sheria, nisingalijua dhambi. Nisingalijua kutamani ni nini kama sheria haikusema, “Usitamani.” 8 bLakini dhambi kwa kupata nafasi katika amri, hii ikazaa ndani yangu kila aina ya tamaa. Kwa maana pasipo sheria, dhambi imekufa. 9Wakati fulani nilikuwa hai pasipo sheria, lakini amri ilipokuja, dhambi ikawa hai, nami nikafa. 10 cNikaona kwamba ile amri iliyokusudiwa kuleta uzima, ilileta mauti. 11 dKwa maana dhambi kwa kupata nafasi katika amri, ilinidanganya, na kupitia katika hiyo amri, ikaniua. 12 eHivyo basi, sheria yenyewe ni takatifu, na amri ni takatifu na ya haki, tena ni njema.

Copyright information for SwhKC